Tuesday, November 11, 2008

Zain yaidhamini THT kuelimisha jamii

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu Zain kutoa sh. milioni 35 kwa kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT) ili kusaidia kuelimisha wanafunzi kujikinga na maambukizo ya UKIMWI. Zain pia ilikabidhi basi kwa kundi hilo. Kushoto ni Meneja wa THT, Rebecca Young na kulia ni Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju.

Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakitumbuiza kwa kuimba katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu Zain kutangaza kutoa sh. milioni 35 na gari aina ya Toyota Hiace kwa kundi hilo kwa ajili ya kutoa elimu kupitia sanaa na maigizo katika programu ya elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika shule za msingi na sekondari nchini.

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe (kulia) akikabidhi ufunguo wa gari aina ya Toyota Hiace kwa Meneja wa Tanzania House of Talent (THT), Rebecca Young ambalo Zain imetoa kwa kundi hilo kwa ajili ya kutoa elimu kupitia sanaa na maigizo katika programu ya elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika shule za msingi na sekondari nchini.


0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP