Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Fabian Massawe (kulia kwake) kukagua eneo la mfereji wa bonde la Mpunga, Msasani jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dampo jipya la Pugu Kinyamwezi wilayani Ilala akiwa katika ziara ya Mkoa wa Dar es salaam . Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira, Batilda Burian.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ukaangaji samaki kwa kutumia gesi katika soko la samaki la Feri wilayani Ilala akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam. Jiko la gesi limeezwa kluwa ni suluhisho la tatizo la Moshi linaloathiri soko hilo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua Kituo Kikuu cha Mabasi yaenedayo Mikoani cha Ubungo jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam March 12, 2009. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Fabian Massawe na kushoto kwake ni Meya wa Jiji la Dar es salaam, Alhaj Adm Kimbisa.
0 comments:
Post a Comment