Monday, October 13, 2008

JK aendelea na ziara Mbeya

Mzee Aidan Mwaisobwa akimpongeza JK baada ya sherehe za kijadi za kumtambua kama mmoja wa machifu wa kabila la Wanyakyusa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Mwakangale,wilayani Kyela jana.Katikati ni Mama Salma Kikwete ambaye amefuatana na Rais katika ziara hiyo ya kikazi ya siku kumi ya mkoa wa Mbeya

JK akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikimba iliyopo wilayani Kyela,Mkoani Mbeya, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.Rais yumo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku kumi kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Dr.Marcelina Chijoriga akimwonesha JK maeneo mbalimbali katika jengo jipya la ofisi ya TRA lililojengwa na Mamlaka hiyo huko,Kasumulu,wilayani Kyela,mpakani mwa Tanzania na Malawi, muda mfupi baada ya Rais kufungua jengo hilo juzi


JK akisoma kitabu katika maktaba ya Taasisi ya Mango Tree,huko wilayani Kyela baada ya kufungua rasmi maktaba ya taasisi hiyo ambayo pia inatoa huduma za elimu na matibabu kwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu.Pembeni ya Rais ni Mkurugenzi wa Taasisi ya The Mango tree Orphan Support Programme Trust Bwana Andilile Sylvester IbrahimJK akiwapungia watoto waliokuwa wakiogelea katika mto Songwe wakati alipolikagua Daraja la mto huko Kasumulu,wilayani Kyela, mkoani Mbeya juzi
JK akikabidhi hundi ya Shilingi milioni mia moja kwa Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha juhudi SACCOS cha Kyela, Bwana Akim Luvanda(wa kwanza kushoto anayepeana mkono na Rais) iliyotolewa kama mkopo kutoka benki ya NMB kwa kikundi hicho.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Uwanja wa michezo wa Mwakangale jana.Wengine katika piacha ni Meneja wa NMB Tawi la Mbeya Bwana John Magigita(Wapili kushoto) na kulia pembeni ya Rais ni katibu wa SACCOS hiyo Bwana Godfrey Sanga (Picha zote kwa hisani ya Freddy Maro wa Ikulu)

JK akiwahutubia mamia ya wakazi wa wilaya ya Kyela katika uwanja wa michezo wa Mwakangale,mjini Kyela juzi mchana


0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP