Friday, November 28, 2008

Zain Yachagua Washindi Wengine

Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuchagua washindi wa muda wa maongezi katika promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya na kulia ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua. Mama wa nyumbani, Julieth Alphonce kutoka Geita aliibuka mshindi wa kwanza na kupata muda wa maongezi wa Sh. 100,000.

Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuchagua washindi wa muda wa maongezi katika promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa na kulia ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua. Mama wa nyumbani, Julieth Alphonce kutoka Geita aliibuka mshindi wa kwanza na kupata muda wa maongezi wa Sh. 100,000.
Mwandishi wa habari wa Chennel Ten, Aneth Kapinga akibonyeza kitufe kumchagua mshindi wa kupata muda wa maongezi wa Sh. 100,000, Julieth Alphonce kutoka Geita wakati wa hafla ya kuchagua washindi wa muda wa maongezi katika promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya, Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa na msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua.


0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP