Thursday, January 15, 2009

Jaji Mkuu wa Tanzania aapisha maofisa wapya wa Mahakama

Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan akimwapisha Bw. John Mgeta kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Rufani Tanzania leo katika ukumbi wa mahakama ya rufaa Tanzania jijini Dar es salaam.Upande wa kulia wa jaji mkuu ni Kaimu jaji kiongozi kanda ya Dar es salaam Aristoclas Kaijage.

Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan akipeana mkono na Bi. Happines Ndesamburo mara baada ya kuapishwa kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Kitengo cha Biashara Mahakama kuu kanda ya Arusha katika sherehe fupi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es salaam.

Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo akiwa na mwanaye Bi Happines Ndesamburo nje ya ukumbi wa Mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Kitengo cha Biashara Mahakama kuu kanda ya Arusha.


Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan(mstari wa mbele katikati) katika picha ya pamoja na maofisa wa mahakama (waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya sherehe fupi ya kuwaapisha kushika nyadhifa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan akimkabidhi hati ya uteuzi Bw. Wilbert Chuma kuwa Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga. Sherehe za makabidhiano hayo zimefanyika leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufani Tanzania, jijini Dar es salaam.
0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP