Tuesday, December 16, 2008

JK ang'ara Msumbiji

JK na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza wa Msumbiji wakitakiana heri kwa kugonganisha glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa katika ikulu ya Maputo ijulikanayo kama Ponta Vermelha jana usiku.

JK akitoa heshima kwa mashujaa ya Msumbiji muda mfupi baada ya kuweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa hao vilivyopo jijini Maputo Msumbiji.Rais kikwete yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

JK akiweka shada la maua leo mchana katika viwanja vya kumbukumbu ya Mashujaa waliomwaga damu wakati wa vita vya ukombozi wa Msumbiji.


Askari wa kike wa jeshi la Msumbiji wakimsindikiza JK kwenda kuweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya Mashujaa mjini Maputo.


JK na ujumbe wake(kushoto) akiwa katika mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Armando Guebuza mjini Maputo leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Msumbiji. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu
0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP