Thursday, January 22, 2009

Waziri Mkuu ndani ya Rocky City

Albino Richard Mpaka wa Kijiji cha Kashekya wilayani Misenyi akichangia katika kikao cha kujadili mbinu za kukomesha mauaji ya albibino kilichojumuisha viongozi wa serikali, dini , vyama vya siasa na albino wa mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa vija katika mji mdogo wa Chato, Januari 20,2009. Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Luambow baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Januari 20,2009, kwa ajili ya kuongoza mkutano wa kujadili mikakati ya kukomesha mauaji ya albino na vikongwe. Kushoto kwake ni mkewe Tunu.

Msanii wa kikundi cha sanaa cha Bujora cha Mwanza, Yassin Anrthony akicheza ngoma ya nyoka wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ili kuongoza kikao cha kujadili mikakati wa kukomesha mauaji ya albino na vikongwe kwenye ukumbi wa vijana katika mji mdogo wa Chato Januari , 2009.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya maalbino wa mkoa wa Kagera baada ya kuongoza kikao cha mkoa huo cha kujadili mbinu za kukomesha mauaji ya maalbino kwenye ukumbi wa vijana katika mji mdogo wa Chato, Januari 20, 20090 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP