Wednesday, February 4, 2009

TIGO YACHANGIA UJENZI WA DARASA KONGOWE SHULE YA MSINGI

Mwalimu wa somo la sayansi wa Shule ya Msingi Upendo, Shakila Mahmoud (kulia) akitoa maelezo jinsi gani wanafunzi wa wanaweza kujifunza masomo mbalimbali kwa kutumia television katika darasa la Shule ya Msingi Kongowe ambalo limewekewa madirisha kwa msaada wa Tigo. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kongowe, Godfrey Semgoja. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kushoto) akishikana mikono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kongowe, Godfrey Semgoja katika ghafla ambayo Tigo ilikabidhi darasa lililowekewa madirisha kwa msaada wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Darasa hilo litatumika kufundisha masomo kwa kutumia television. Kulia ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Augustine Emanuel.

0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP