Monday, March 16, 2009

Gazeti jipya la Jamii

Pichani ni jina la gazeti jipya la ' Kwanza Jamii' linalotarajiwa kuonekana nchini kote kuanzia Machi 31, 2009.

Ni jarida la uchambuzi wa masuala yanayohusu na kuigusa jamii.

Haya ni pamoja na siasa,uchumi, elimu, michezo na utamaduni.

Kuna masuala mtambuka pia kama vile mazingira,jinsia na UKIMWI/VVU.

Jarida hilo litakuwa likitoka kila Jumanne ya wiki. Linamilikiwa na Ikolo Investiment Co. Ltd ambao awali walimiliki na kuchapisha GoziSpoti.

Katika muda si mrefu kutoka sasa tutawaletea, kupitia blogu hii, majina ya baadhi yawachambuzi watakaoandikia gazeti hilo.

Kwa sasa tunaandaa bango la ' Kwanza Jamii' litakalotundikwa hapo juu.

Maggid
Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Jumapili, Machi 15, 2009.

0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP