Monday, September 29, 2008

Zain yatangaza shule 26 zitakazopewa vitabu

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe akimkabidhi vitabu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote wilayani humo jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Zain ilichezesha bahati nasibu na kupata shule 26 za Tanzania zitakazopewa vitabu katika mradi wa Build Our Nation (BON).

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuchagua moja ya shule 26 za mikoa yote ya Tanzania katika bahati nasibu ya mradi wa Build Our Nation (BON) wa Zain wilayani Ilemela, Mwanza mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote

Fundi wa kompyuta wa Zain Tanzania, Adrian Msuya akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuchagua moja ya shule 26 za mikoa yote ya Tanzania katika bahati nasibu ya mradi wa Build Our Nation (BON) wa Zain wilayani Ilemela, Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote, Ofisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Mwanza, Stella Nyala na Meneja Mauzo wa Zain Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya.



Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibinza wilayani Ilemela, Mwanza wakiimba kwaya wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ilipofanya bahati nasibu ya kuchagua shule 26 za Tanzania zitakazopata vitabu katika mradi wa Build Our Nation (BON) wilayani Ilemela, mwishoni mwa wiki



Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote (kulia) akikabidhi vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Igagala ya Tabora, Eliezer Ukwai wilayani Ilemela, Mwanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe na wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Ibinza, James Chisanda. Zain ilichezesha bahati nasibu na kupata shule 26 za Tanzania zitakazopewa vitabu katika mradi wa Build Our Nation (BON).





Mtendaji wa Mauzo na Utawala wa Zain Mwanza, Brenda Nkong'wanzoka (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuchagua moja ya shule 26 za mikoa yote ya Tanzania katika bahati nasibu ya mradi wa Build Our Nation (BON) wa Zain wilayani Ilemela, Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe, Fundi wa kompyuta wa Zain, Adrian Msuya, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote, Ofisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Mwanza, Stella Nyala na Meneja Mauzo wa Zain Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya.




0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP