Thursday, December 18, 2008

JK ahitimisha ziara yake Msumbiji

Mtaalamu wa utafiti katika kituo cha ukaguzi wa samaki katika bandari ya Maputo,chini Msumbiji akitoa maelezo kwa JK juu ya ukaguzi na uatafiti wa samaki unaofanywa na kito hicho.Msumbiji inauza samaki wake katika nchi za Ulaya



Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Diplomasia mjini Maputo Dr.Patricio Jose akimpa zawadi ya kinyago JK baada ya kutoa mhadhara katika chuo hicho jana juu ya Mtazamo wa Tanzania Juu ya Jumuiya ya Maendelo ya Uchumi Kusini mwa Afrika SADC.Rais kikwete leo amehitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Msumbiji na tayari amerejea jijini Dar


Mtaalamu wa Zao la Mpunga katika kituo cha Utafiti wa kilimo cha Umbeluzi,Boane nje kidogo ya jiji la Maputo Bwana Marcos Langa akitoa maelezo kwa JK juu ya uzalishaji wa mbegu bora ya zao hilo.Kituo hicho kina ushirikiano wa karibu na Vituo cha utafiti wa mazao vya Naliendele, Mtwara na Ifakara mkoani Morogoro



JK akitoa mhadhara kwa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Diplomasia mjini Maputo jana juu ya Mtazamo wa Tanzania Juu ya Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC.




0 comments:

About This Blog

Blog Archive

Waliotembelea ukurasa huu

free counter

  © The Professional Template Under Dullonet Tanzania @ 2008

Back to TOP