MUSWAADA WA SHERIA YA UTALII NA WANYAMAPORI AFRIKA MASHARIKI WAJADILIWA NA WADAU
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Rwanda Bi. Patricia Hajabakiga akifafanua jambo wakati wa warsha ya kukusanya maoni ya muswaada mpya wa sheria ya Utalii na Wanyamapori uliowasilishwa na mbunge Safina Kwekwe kutoka kenya ili ujadiliwe na wadau wa nchi zote washiriki wa jumuiya hiyo kabla ya kuupitishwa na bunge hilo na wakuu wa nchi husika na kuwa sheria kamili itakayosimamia masuala ya Utalii na wanyamapori kwa pamoja katika nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki katikati ni mwenyekiti wa warsha hiyo na mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. George Nangare anayefuata pia ni Mbuge wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania Photnatus Masha warsha hiyo imefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini na iliandaliwa kwa pamoja na TTB na EAC
0 comments:
Post a Comment